Dodoma FM

Wafanyabiashara wa vyakula watakiwa kufuata sheria ya Afya ya jamii

2 February 2022, 4:05 pm

Na; Benard Filbert.

Idara ya afya katika jiji la Dodoma imeanza oparesheni ya ukaguzi wa maeneo yanayotumika kuuzia vyakula na vinywaji  katika kata zote lengo ikiwa kuwataka wauzaji hao kufuata sheria ya afya ya jamii ya mwaka 2009.

Hayo yameelezwa na afisa afya wa jiji la Dodoma Abdallah Mahiya wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu ukaguzi huo ambao umeanza hivi karibuni.

Amesema lengo la  kampeni hiyo nikutaka kila mfanyabiashara wa chakula na sehemu za kuuzia vinywaji kuhakikisha anafuata taratibu zote kwa mujibu wa sheria ili kuepusha kuathiri afya ya watumiaji.

Ameongeza kuwa kampeni hiyo inajiri kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wa sehemu hizo kuchukulia kawaida na kutokuzifuata kanuni za afya ambazo zinawataka kufanya hivyo.

Baadhi ya wafanyabiashara wa chakula na sehemu za kuuzia vinywaji wamesema opereshani hiyo itasaidia wafanyabiashara wengi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kufuata sheria ya afya na kanuni zake.

Idara ya afya ofisi ya jiji la  Dodoma imeanza kampeni hiyo katika maeneo ya pembezoni mwa jiji ili kufanya ukaguzi kwa wafanyabiashara wote lengo kuwahimizi kufuata taratibu zote za afya wakati wakiwa wanafanya biashara zao.