Dodoma FM

Rais Samia Suluhu Hassan jana alifanya ziara na kukagua ujenzi wa Barabara ya Mwendokasi ya Mbagala

2 June 2021, 6:42 am

Na; Mariam Kasawa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Kwa Azizi Ali mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kukagua mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi katika barabara ya Kilwa.

Wananchi wa Mtongani na Kwa Azizi Ali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasalimia wakati akikagua ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo haraka (BRT) Awamu ya Pili (Mwendokasi) katika barabara ya Kilwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mbagala mkoani Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi katika barabara ya Kilwa.

Wananchi wa Mbagala wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza nao wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi katika barabara ya Kilwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipewa maelezo kuhusu mradi wa Soko la Kisutu mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Sokoni hapo.