Wakazi Ihumwa A walalamikia kukosekana kwa barabara za mtaani
7 September 2026, 16:43

Diwani wa Kata ya Ihumwa, Edwadi Magawa, amesema zoezi la ukarabati wa barabara za mitaa linaendelea kwa awamu, hivyo wananchi wanapaswa kuwa wavumilivu kwani litafika katika kila mtaa.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa Mtaa wa Ihumwa A wamehoji kukosekana kwa barabara za mtaani katika eneo hilo, wakati zoezi la ufunguzi na ukarabati wa barabara likiendelea katika mitaa mingine ndani ya Kata ya Ihumwa.
Wakizungumza kuhusu changamoto hiyo, baadhi ya wananchi wamesema ukosefu wa barabara za mtaani unafanya usafirishaji kuwa mgumu na kuathiri shughuli zao za kila siku, hivyo kuiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kutengeneza barabara hizo.
Wamesema kuwa uwepo wa barabara za mtaani utarahisisha usafirishaji na kuongeza ufanisi wa shughuli mbalimbali zinazofanyika katika eneo hilo.