Dodoma FM

Umiliki halali wa ghala Matui wazua mgogoro

13 July 2026, 15:52

Picha ni wananchi wa kijiji cha Matui wilayani Kiteto wakiwa nje ya ghala hilo.Picha na Kitana Hamis.

Hii hapa tarifa yake  kitana Hamisi kutoka wilayani Kiteto  Mkoani Manyara.

Na Kitana Hamis.

Mvutano wa umiliki wa ghala lililopo Kijiji cha Matui, Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, umeendelea kushika kasi huku wananchi na Chama cha Ushirika cha Matui (Matui AMCOS) wakitofautiana kuhusu mmiliki halali wa ghala hilo.

Wananchi wameeleza kuwa walihudhuria mkutano waliotarajia kupata ufafanuzi wa suala hilo, lakini waliondoka bila majibu baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto kutofika katika mkutano huo.

Wameiomba serikali kuingilia kati na kutoa ufafanuzi wa mwisho ili kumaliza sintofahamu iliyodumu kwa muda mrefu.

Diwani wa Kata ya Matui amesema mvutano huo unaendelea kuathiri maendeleo ya eneo hilo, akisisitiza umuhimu wa suala hilo kushughulikiwa haraka ili kurejesha utulivu.

Picha ni mwenyekiti wa kijiji cha Matui akiongea katika kikao hicho.Picha na Kitana Hamis.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Matui amesema walishawasilisha malalamiko yao kwa Mkuu wa Wilaya lakini bado hawajapata majibu ya kina.

Kwa upande wake, Meneja wa Chama cha Ushirika cha Matui (Matui AMCOS), amesema ghala hilo ni mali ya chama hicho na lilijengwa mwaka 1989, huku akieleza kuwa tayari hatua zilishachukuliwa na uongozi wa wilaya kuhusu suala hilo.

Akizungumza kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Remidius Mwema, amesema suala hilo tayari amelishughulikia.

Sauti ya kina Kitana Hamis.