Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuendelea kushiriki usafi wa mazingira

26 October 2026, 17:50

Picha ni baadhi ya wakazi wa mtaa wa Mathias wakifanya usafi mtaani hapo.Picha na Anwary Shaban.

zoezi hilo la usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma linatekelezwa kupitia kampeni ya Work and Pick, inayo lenga kuhamasisha wananchi kufanya usafi.

Na Anwary Shaban.

Wakati mvua kubwa za El Niño zikitarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, wananchi wa mtaa wa Mathiasi, Kata ya Miyuji jijini Dodoma, wameungana na Taasisi ya Green Samia Foundation kufanya usafi wa mazingira kwa lengo la kuzuia milipuko ya magonjwa na kupunguza athari zinazo weza kusababishwa na mvua hizo.

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha usafi wa mazingira na kuhamasisha jamii kuchukua tahadhari mapema kwa kusafisha maeneo yanayo zunguka makazi yao, kuondoa taka na kuhakikisha mazingira yanakuwa salama.

Akizungumza na Taswira ya Habari jijini Dodoma, Bakari Hassani, mratibu wa Green Samia Foundation amesema taasisi hiyo inasimamia usafi wa mazingira na inaona umuhimu wa wananchi kushirikiana katika kuyatunza ili kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua.

Picha ni baadhi ya wakazi wa mtaa wa Mathias wakifanya usafi mtaani hapo.Picha na Anwary Shaban.

Aidha, amesema zoezi hilo la usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma linatekelezwa kupitia kampeni ya Work and Pick, inayo lenga kuhamasisha wananchi kufanya usafi na kuhimiza taasisi nyingine kuunga mkono juhudi hizo kwa manufaa ya jamii.

Kwa upande wake, Daudi Mahinyila, balozi wa Shina Namba 4 katika mtaa wa Matiasi, , amesema wananchi wameamua kujitokeza kushiriki shughuli za usafi ili kujiandaa kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño, huku akiwahimiza wananchi wengine kuendelea kutunza mazingira yao.

Ripoti na Anwary Shaban.