Dodoma FM

Wanandoa watakiwa kuwa wawazi katika masuala ya fedha

19 October 2026, 16:38

Ni muhimun wanandoa kujenga uaminifu ndani ya ndoa na kuepusha migogoro.Picha na Mtandao.

Washauri wa masuala ya ndoa na familia wanafafanua kuwa ustawi wa nyumba unategemea zaidi uwezo wa wana ndoa kusimamia mipango yao ya kiuchumi.

Na Andrew Kyuki.

Uwazi na ukweli katika masuala ya fedha baina ya mke na mme vimetajwa kuwa silaha kuu ya kujenga maelewano, amani na maendeleo endelevu ndani ya familia na ndoa.

Hayo yameelezwa na Bwana Joel Masume, mshauri wa masuala ya ndoa na familia kutoka Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, amesisitiza umuhimu wa wanandoa kuweka wazi taarifa zinazohusu vipato vyao ili kujenga uaminifu ndani ya ndoa na kuepusha migogoro.

Katika hatua nyingine Masume ametoa angalizo kwa wazazi na ndugu wa pande zote mbili kutokuingilia masuala ya kiuchumi ya wanandoa, lengo likiwa ni kulinda heshima na kuweka mipaka inayochochea uwajibikaji na maendeleo ya familia.

Nao baadhi ya wananchi kutoka kata ya Nyasubi wameto mitazamo yao kuhusu michango ya kifedha na umuhimu wa ushirikiano wa pamoja kati ya baba na mama katika kukuza uchumi wa familia.

Ripoti ya Andrew Kyuki.

Washauri wa masuala ya ndoa na familia wanafafanua kuwa ustawi wa nyumba unategemea zaidi uwezo wa wana ndoa kusimamia mipango yao ya kiuchumi kwa pamoja, kuepuka ushawishi wa nje na kulinda faragha ya kifedha ili kujenga misingi thabiti inayozuia mianya yote ya migogoro na kukuza maelewano ya kudumu.