Uhaba wa maji wapelekea wanafunzi kuchelewa masomo Mbelezungu
6 November 2026, 17:27

Huduma ya maji pia inakosekana shuleni hali inayo walazimu wanafunzi kutumia muda mrefu kutafuta maji na kuchelewa masomo.
Na Victor Chigwada.
Kukosekana Kwa huduma ya maji katika kitongoji cha Mbelezungu B Kata ya Majelelo Wilayani Chamwino umepelekea kukwamisha shughuli mbalimbali pamoja kuathiri muda wa wanafunzi shuleni.
Wananchi hao Mbelezungu wameiomba Serikali kutatua changamoto hiyo ili kuondokana na matumizi ya maji ya visima vya asili pamoja na kuondokana na adha ya wanafunzi kutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kukaa darasani kwaajili ya masomo.
George Isaya mwenyekiti wa Kijiji Cha Mbelezungu amekiri ukosefu wa maji katika eneo hilo ambapo amesema huduma ya maji pia inakosekana shuleni hali inayo walazimu wanafunzi kutumia muda mrefu kutafuta maji na kuchelewa masomo.
Nao baadhi ya wanafunzi walio hitimu katika shule ya msingi Mbelezungu wamesema changamoto ya maji kijijini hapo inawathiri hasa wasichana Kwani baadhi hukutana na ukatili wanapo kuwa wakitembea kutafuta maji,