Wananchi washauriwa kujenga utamaduni wa kuweka akiba
8 October 2026, 17:19

Wananchi wametakiwa kujenga utamaduni wa kuweka akiba katika maisha ya kila siku ili kuwa na uwezo wa kukabiliana na ongezeko la gharama za maisha na kuhakikisha wanamudu mahitaji muhimu kama chakula, malazi na huduma nyingine za msingi.
Na Daniel Njau.
Baadhi ya wananchi wameeleza namna wanavyokabiliana na gharama za maisha, wakisisitiza umuhimu wa kupanga matumizi ya fedha ili kuhakikisha mahitaji muhimu ya familia yanapatikana.
Mshauri wa masuala ya fedha na biashara, Bwana Joel MKede, amesema jamii inapaswa kujenga utamaduni wa kuweka akiba hata kama ni kiasi kidogo, ili kuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto za kifedha zinazoweza kujitokeza na kukidhi mahitaji muhimu.
Amesema pia wananchi wanapaswa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza sehemu ya kipato katika akiba na uwekezaji, hatua ambayo inaweza kusaidia kuboresha maisha yao, familia na jamii kwa ujumla.