Dhana potofu zinavyokwamisha matumizi ya uzazi wa mpango
28 October 2026, 17:18

Kwa mujibu wa tafiti kutoka Afya ya Uzazi na Viashiria vya Malaria Tanzania wa mwaka 2022, asilimia 21 ya wanawake walio olewa walikuwa na uhitaji ambao haujatimizwa wa huduma za uzazi wa mpango, jambo linalo onesha umuhimu wa kuendelea kuimarisha elimu na upatikanaji wa huduma hizo.
Na Mwanaid Mpetu.
Dhana potofu zinazo sambazwa katika jamii kuhusu njia za uzazi wa mpango zimetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazo kwamisha matumizi sahihi ya huduma hizo.
Baadhi ya wananchi wamekuwa na hofu ya kutumia uzazi wa mpango kutokana na uelewa mdogo walio nao juu ya matumizi ya njia hizo pamoja na dhana potofu zilizo jengeka kwa baadhi ya watu kuwa njia hizo zina madahara.
Taswira ya habari imezungumza na Dkt. Francis Mbwilo kutoka chama cha uzazi na malezi Tanzania UMAT ambapo amesema ni muhimu jamii kupata elimu sahihi kutoka kwa wataalamu wa wa afya badala ya kutegemea taarifa ambazo hazija thibitishwa na wataalamu wa afya.