Recent posts
16 June 2023, 14:28
Vijana Kikuyu waipongeza serikali kuwasogezea huduma, elimu ya Afya
Katika kata ya Kikuyu Kaskazini watu 103 wamepata elimu na kupima masuala ya lishe ambapo asilimia 12.6% walibainika na utapiamlo, watu 80 wakipata elimu juu ya Magonjwa yasiyo ya kuambukiza na Bonanza hilo linatarajiwa kuhitimishwa siku ya kesho Jumamosi Makulu.…
16 June 2023, 13:54
Vijana Kongwa wapokea bonanza la afya
Afisa lishe wilaya Kongwa Bi. Maria Haule amesema vijana lika balehe wakike wanatakiwa kujenga utaratibu wa kula vyakula vinavyoongeza damu ili kusaidia kurudisha damu inayopotea wakati wa hedhi. Na Bernadetha Mwakilabi. Wilaya ya Kongwa imepongeza na kushukuru wizara ya afya…
16 June 2023, 13:28
Siku ya mtoto Afrika huadhimishwa kuangalia maslahi mapana ya watoto
Siku ya mtoto wa Afrika inaadhimishwa kwa lengo la kuangalia maslahi mapana ya watoto wa Afrika na huwapasa watu wazima kujitolea kwa hali na mali ili kushughulikia changamoto zinazokabili watoto katika bara zima la Afrika pamoja na kulindwa dhidi ya…
16 June 2023, 12:43
Vijana Bahi wapigwa marufuku kucheza pool table muda wa kazi
Yeyote atakayekutwa anacheza pool table muda wa kazi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na atachukuliwa kama mzurulaji na atashtakiwa kisheria. Na Bernad Magawa. Jeshi la polisi wilayani Bahi limepiga marufuku vijana kucheza pool table muda wa kazi na kusema…
14 June 2023, 18:00
Vituo vya afya vyatakiwa kununua majokofu ya kuhifadhia mazao ya damu
Tanzania leo imeungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha siku ya Wachangia Damu Duniani ambayo inalenga kuongeza ufahamu na kuwashukuru wafadhili wa damu wa hiari, wasiolipwa kwa zawadi zao za kuokoa maisha. Na Mindi Joseph. Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu…
14 June 2023, 16:53
Dodoma: Wafanyabiashara watakiwa kujiunga UBIMIDO
Umoja wa wafanyabiashara waendao mnadani umekuwa na umuhimu mkubwa hususani katika suala la kuwasaidia wafanyabiashara katika kusaidiana kwenye masuala mbalimbali. Na Thadei Tesha Wafanyabiashara jijini Dodoma wametakiwa kujiunga katika umoja wa wafanyabiashara UBIMIDO ili waweze kupata fursa za kujikwamua kiuchumi…
14 June 2023, 15:24
Asilimia 97 watumiaji dawa wamefanikiwa kufubaza virusi vya Ukimwi
Waziri Ummy ametoa wito kwa Watanzania kwenda kupima kujua hali zao lakini kwa ambao wanajua hali zao dawa za UKIMWI zipo na zinatolewa bila malipo na vipimo vya kujipima mwenyewe vipo kwahiyo Watanzania wajitokeze kupima ili tutokomeze UKIMWI ifikapo mwaka…
14 June 2023, 13:50
Wakazi Msisi waipongeza serikali ujenzi maabara shule ya sekondari Msisi Juu
Maabara hizo zitachochea wanafunzi wengi wa shule hiyo ya Msisi Juu kupenda masomo ya sayansi. Na Bernad Magawa . Wananchi wa kata ya Msisi wilayani Bahi wameishukuru serikali kwa kujenga maabara za masomo ya sayansi kwenye shule ya sekondari Msisi…
14 June 2023, 13:14
Bahi: Wakandarasi watakiwa kukamilisha, kukabidhi miradi ya maendeleo Juni 15
SSP Idd Abdala amesema Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu, hivyo ni vema miradi yote ikakamilika kwa wakati. Na Bernad Magawa. Serikali wilayani Bahi mkoani Dodoma imewaagiza mafundi wote wanaojenga miradi ya maendeleo miundombinu ya…
14 June 2023, 12:10
Viongozi kanisa katoliki waaswa kudumisha amani, baraka
Viongozi wamekumbushwa kuwa na mshikamo ili kuepusha migongano mbalimbali isiyokuwa ya lazima. Na Bernad Magawa. Viongozi wa kanisa jimbo kuu katoliki Dodoma wameaswa kuwa wasikilizaji wazuri wa shida za wale wanaowaongoza huku wakikumbushwa kufanya utafiti wa kina kabla wa kutolea…