Dodoma FM

Bei ya mafuta ya alizeti yapaa

11 January 2021, 12:45 pm

Na,Shani,

Dodoma

Imeelezwa kuwa kupanda kwa bei ya mafuta ya kula hususan ya alizeti kumechangiwa na mvua kubwa iliyonyesha msimu uliopita.
Hayo yameelezwa na wafanyabasara katika soko la Majengo jijini Dodoma wakati wakizungumza na Dodoma Fm ambapo wamesema alizeti imeadimika kutokana na wakulima wengi kutopata mavuno mazuri msimu uliopita baada ya mvua kuziharibu shambani.

Nao baadhi ya wanunuzi wa mafuta jijini hapa wameiomba serikali kuwekeza katika kilimo cha zao hilo ili kuepuka kutegemea mafuta kutoka nje kwa asilimia kubwa ambayo mara nyingi huuzwa bei ghali.
Kwa mwaka Tanzania inazalisha tani 200,000 za mafuta ya kula ingawa mahitaji yake ni tani 500,000 hivyo kuagiza tani 300,000 kutoka nje hasa mataifa Asia zaidi Malaysia na Indonesia.