Dodoma FM

Uvutaji wa sigara na shisha wachangia magonjwa ya moyo kwa vijana

9 April 2026, 17:25

Mkurugenzi Mtendaji wa Jakaya Kikwete Cardiac Institute, Dkt. Peter Kisenge.Picha na Habari maelezo.

Jakaya Kikwete Cardiac Institute(JKCI) ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa mwaka 2015, ikiwa ni hospitali maalum ya kitaifa inayo jihusisha na huduma za magonjwa ya moyo. Taasisi hiyo hutoa huduma za matibabu ya moyo, huduma maalum za kibingwa, hufanyatafiti za magonjwa ya moyo pamoja na kutoa elimu kwa jamii kuhusu kinga na tiba ya magonjwa hayo.

Na Bennard Filbert.

Unywaji wa pombe  pamoja na uvutaji wa sigara umetajwa kuwa miongoni mwa sababu kuu zinazo sababisha ongezeko la magonjwa ya moyo, hususani kwa wanaume.

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Jakaya Kikwete Cardiac Institute, Dkt. Peter Kisenge, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Mtumba  jijini Dodoma.

Amesema kuwa mtindo wa maisha usiozingatia afya, ikiwemo matumizi ya pombe kupita kiasi na uvutaji wa sigara, ni miongoni mwa vichocheo vikuu vinavyopelekea wanaume wengi kupata magonjwa ya moyo.

Aidha, Dkt. Kisenge ameeleza kuwa nchi zenye uchumi mdogo zinaendelea kukabiliwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa moyo kutokana na changamoto ya upatikanaji mdogo wa vifaa tiba, hali inayosababisha kuchelewa kwa uchunguzi na matibabu ya mapema.

Sauti ya Dkt. Kisenge.

Katika hatua nyingine, amewashauri wanawake wajawazito kuzingatia lishe bora wakati wa ujauzito ili kupunguza hatari ya watoto kuzaliwa na matatizo ya moyo.

Sauti ya Dkt. Kisenge.