Dodoma FM

Watatu wajeruhiwa kwa ajali ya gari Mpwapwa

20 March 2026, 16:45

Picha ni gari hilo likiwa limegonga nyumba katika eneo hilo.Picha na Steven Noel.

Gari hiyo ambayo ilikuwa ikiendeshwa kwa mwendo kasi iliacha njia ghafla na kuvamia makazi ya watu.

Na Steven Noel

Watu watatu wamenusurika  kufa katika ajali baada ya gari aina ya lori lenye usajili namba  T676DFC lililobeba kokoto kuacha njia na kugonga makazi ya watu katika mtaa wa Hazina namba 30  wilayani Mpwapwa.

Wakiongea na Taswira ya Habari, mashuhuda wa ajali hiyo  wamesema gari hiyo ambayo ilikuwa ikiendeshwa kwa mwendo kasi iliacha njia ghafla na kuvamia makazi ya watu yaliyo karibu na barabara hiyo.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo diwani wa kata ya hazina Bw.Emanuel Ndule amesema watu watatu wamejeruhiwa katika ajali hiyo na tayari wamepelekwa hospitali kwaajili ya matibabu.

Sauti ya kina