Dodoma FM
Dodoma FM
26/02/2026, 11:57

Wananchi wa eneo hilo wameishukuru serikali kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa sekondari hiyo.
Na Victor Chigwada.
Ujenzi wa shule ya sekondari Mapinduzi A umekuwa mkombozi Kwa wanafunzi wa mtaa huo ambao hapo awali walilazimika kutembea umbali mrefu hadi shule ya sekondari Ngh’ongh’ona .
Baadhi ya wazazi walilazimika kuwapangia vyumba watoto wao karibu na shule hali iliyo hatarisha usalama hasa kwa watoto wa kike .
Golden Mathayo mwenyekiti wa mtaa wa Mapinduzi A ameishukuru Serikali Kwa kutoa fedha za kujenga sekondari hiyo ambayo awali ilikuwa ni changamoto Kwa wanafunzi wa mtaa huo.
Mathayo ameongeza kuwa uwepo wa shule hiyo ya sekondari umepunguza gharama za wazazi kuwapangishia watoa wao vyumba lakini zaidi imekuwa ni fursa ya kuwalea watoto wao Kwa ukaribu zaidi.