Dodoma FM

Wakazi Chiona waiomba serikali kuwajengea zahanati

11 February 2026, 12:40 pm

Ukosefu wa Zahanati umekuwa kero kubwa kwa wananchi. Picha na mtandao.

Chilewa ameongeza kuwa hata hivyo upo mpango wa ujenzi wa zahanati mpya ambayo ilianzishwa na wananchi hivyo wanasubiri ujenzi ambao utaondoa kilio Cha wananchi hao.

Na Mariam Kasawa.

Wananchi wa kijiji cha Chiona Wilaya ya Chamwino wameiomba Serikali kutatua kero ya ukosefu wa zahanati kijijini hapo ili kuepusha adha ya kufuata huduma za afya umbali mrefu.

Wakizungumza na taswira ya habari wamesema kumekuwa na changamoto ya kupata tiba Kwa wagonjwa sambamba na Mahudhurio ya kiliniki kwa akina mama wajawazito kuwa ya shida hali inayopelekea wakati mwingine wamama wajawazito kujifungulia nyumbani.

Sauti za wananchi.

Akieleza Matarajio mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Vicent Chilewa amesema suala la matibabu limekuwa ni kero kubwa Kwa wananchi na wakati mwingine kimekuwa likiwakatisha tama ya kwenda kutibiwa na kubaki majumbani

Sauti ya Bw.Vicent Chilewa.