Dodoma FM
10 wanusurika ajali ya gari Dodoma
4 November 2024, 7:34 pm
Na Lilian Leopord.
Hali za majeruhi 10 ambao wamenusurika katika ajali iliyotokea Novemba 3 katika Kata ya Makulu jijini Dodoma na kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma imeendelea kuimarika.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Loveness Meena anaeleza jinsi walivyowapokea majeruhi hao na hatua za haraka walizozichukua.
Aidha baadhi ya majeruhi wanaelezea chanzo cha ajali hiyo na jinsi walivyopata msaada wa haraka toka kwa wananchi.
Aidha majeruhi hao wameiomba mamlaka husika kuwachukulia hatua madereva ambao wanakiuka sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali zinazosababishwa na uzembe wa madereva .