Dodoma FM
Matumizi ya mfumo 5s Kaizen waonesha matunda sekta ya afya
3 October 2024, 8:10 pm
Na Mindi Joseph.
Utekelezaji wa mfumo wa 5s Kaizen katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma General umechangia utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Muuguzi Mfawidhi wa hospitali hiyo Stanley Mahundo anasema kuwa mfumo huo ulianza kutumika mwaka 2015 .
Mshauri Mwandamizi wa mradi huo unaoimarisha huduma za mama na mtoto katika ngazi ya Rufaa ya Mkoa Dodoma Farisi Masaule anasema ubora wa utoaji wa huduma kwa wananchi umeimarika.
Mfumo wa 5s Kaizen unaotekelezwa na Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan JICA umeboresha huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa wananchi.