Dodoma FM

Elimu utambuzi noti bandia yahitajika zaidi

25 September 2024, 8:27 pm

Na Fred Cheti

Wananchi jijini Dodoma wameomba kupatiwa elimu zadi  juu ya utambuzi wa noti bandia ili  kuepukana na changamoto za noti hizo katika mzunguko wa shilingi.

Jamii kwa sasa imekumbwa na changamoto ya uwepo wa noti bandia kunakofanywa na baadhi ya watu wanaotumia noti hizo kufanya utapeli katika maeneo mbalimbali ya huduma.

Wananchi mameiomba serikali kupitia taasisi zake za kifedha  itoe elimu kwa jamii ili iweze kuwa na uelewa juu ya noti hizo.

Sauti za wananchi

Katika kusaidia utambuzi wa alama muhimu katika baadhi ya noti Kuu za Tanzania Benki Kuu ya Tanzania imetoa makala inayoeleza alama muhmu za utambuzi wa noti halali ambazo si rahisi kupatikana katika noti bandia.

Makala ya Benki Kuu ya utambuzi wa noti bandia