Dodoma FM

Serikali yaanza kuwachimbia visima wakulima wadogo Manchali

28 May 2024, 6:26 pm

Mradi huu wenye ekari 21 utawanufaisha wakulima katika uzalishaji kupitia kilimo cha umwagiliaji.Picha na Mindi Joseph.

Pamoja na hayo Wizara ya kilimo itahakikisha inawasaidia Wakulima wadogo waliopo katika mradi huo kupima mashamba yao ili wapate hati.

Na Mindi Joseph.
Serikali imeanza utekelezaji wa mradi wa kuwachimbia visima wakulima wadogo katika kijiji cha manchali jijini Dodoma ili waweze kuzalisha bila kutegemea mvua.

Miongoni mwa Wakulima wanatarajia kunufaika wameishukuru wizara ya kilimo kwa kutekeleza mradi huo ambao utawawezesha kuzalisha kwa tija.

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema mradi wa visima kwa wakulima wengi hawakuamini kama utakuwa na mchango kwa wakulima na kuwaomba wakulima wasiuze ardhi zao.