Dodoma FM

Migogoro ya ndoa chanzo cha watoto wanao ishi mtaani

13 Aprili 2026, 16:28

Picha ni Afisa ustawi wa halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa  Bi. Rose Sichilima.Picha na Steven Noel.

Kwa mwaka 2026 Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni  malezi  na ulinzi wa mtoto ni WAJIBU wetu sote.

Na Steven Noel.

Jamii imeshauriwa kuchukua hatua dhidi  ongezeko  la watoto wanaotumikishwa mitaani pamoja na ongezeko la watoto wa mitaani   linalozidi kuongezeka siku hadi Siku.

Wito huo umetolewa na kaimu Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa  ambae ni katibu tarafa Mima Bi Arene Milinga kwenye kilele cha maadhimisho ya  ya Siku  ya kimataifa  ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani ,

Amesema kuwa  tafiti na taarifa mbalimbali zinadai migogoro  ya ndoa pamoja  umaskini wa kipato cha familia ni chanzo  moja wapo cha watoto wanaotumikishwa mitaani .

Aidha Afisa ustawi wa halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa  Bi. Rose Sichilima  amesema tangu maadhimisho hayo yaanze tarehe mosi   Kwa wilaya ya Mpwapwa wamewabaini watoto 235 wakiwa wasichana 135 na wavulana 89 wanaotumikishwa kazi mbalimbali .

Naye Afisa maendeleo ya Jamii kitengo cha watoto Bwana Zakaria Kiondo  amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuikumbusha Jamii  juu ya kuchukua hatua dhidi ya utoaji wa Haki za malezi  Kwa watoto wanaoishi na kutumikishwa mitaani.

Sauti ya kina Noel.