Dodoma FM

Mwanaume anaweza kuzungumzia ukatili wa kijinsia anaofanyiwa?

13 Aprili 2026, 10:53

Ingawa ukatili wa kijinsia anaweza kufanyiwa mtu yeyote, kundi la wanawake na watoto ndio wahanga wakubwa wa ukatili wa kijinsia. Picha na mtandao.

Matendo ya ngono yatakayosababishwa kwa maneno au matendo na mtu aliye na madaraka katika sehemu ya kazi au sehemu nyingine yoyote, atakuwa ametenda kosa la udhalilishaji wa kijinsia.

Na Mariam Kasawa
Umoja wa Mataifa unafafanua kuwa ukatili wa kijinsia ni kitendo chochote anachofanyiwa mtu yeyote awe mwanamke, mwanaume au mtoto, kinacholenga kumuumiza kimwili au kiutu.
Ingawa ukatili wa kijinsia anaweza kufanyiwa mtu yeyote, kundi la wanawake na watoto ndio wahanga wakubwa wa ukatili wa kijinsia.
Kwa Mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini 2004; Sura ya 138 (D) ya kanuni za adhabu, 1945.
Anayekutwa na hatia ya kufanya hivyo, ataweza kupata kifungo cha hadi miaka mitano, au faini isiyozidi shilingi laki mbili au vyote kwa pamoja na pia anaweza kupewa amrisho la kulipa fidia kwa aliyeathirika kama itakavyo amriwa na mahakama.