Dodoma FM
Dodoma FM
9 April 2026, 13:08

Kwa upande mwingine Halfan ameweka wazi kuwa tume hiyo kwa mujibu wa Katiba ya nchi ibara ya 129 mpaka ibaraya 131 zime ainisha majumu kwa ujumla na namna ambavyo utekelezwaji wake ulivyo na kupitia utekelezwaji huo jamii hupata maendeleo kwa kushirikiana na viongozi pasipo kuvunja haki.
Na Jerome John.
Jamii imetakiwa kushirikiana na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kutoa taarifa pindi uvunjifu wa haki zozote za binadamu unapo tokea.
Akizungumza mapema leo naTaswiraya Habari mchunguzi mkuu msaidizi Halfan Mbotea kutoka Tume hiyo amesema kumekuwepo na viashiria au matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu nchini hivyo tume hiyo imekuwa ikifanya uchunguzi na kuhakikisha hatua mbalimbali zinachukuliwa na wahusika kuwajibishwa.
Aidha afisa huyo amebainisha kuwa kutokana na baadhi ya wanajamii kutokuwa na uelewa wa haki zao wamekuwa wakipoteza haki na wakati mwingine kutendewa ndivyosivyo na kushindwa kutoa taarifa katika tume hiyo.