Dodoma FM

Upungufu wa dawa zahanati ya Manchali kilio kwa wananchi

8 April 2026, 12:26

Upungufu wa dawa wa mara kwa mara umekuwa ukiwakatisha tama wananchi wa kijiji hicho.Picha na Mtandao.

Wameiomba serikali kupitia wizara ya Afya kuwasaidia dawa za kutosha katika zahanati hiyo ili wananchi waepukane na adha kwenda kununua dawa nje ya hospitali.

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa Kijiji Cha Manchali A wameiomba Serikali kuboresha upatikaji wa huduma ya dawa katika zahanati yao ili kuondokana na adha ya wananchi wa eneo hilo kukosa dawa kila wapokwenda kupata matibabu.

Wakizungumza na Taswira ya habari wananchi hao wamesema kuwa licha ya zahanati hiyo kuwa na wahudumu wa afya wanao jitahidi kutoa huduma kwa wakati lakini kikwazo cha ukosefu wa dawa wa mara kwa mara umekuwa ukiwakatisha tama wananchi.

Mwenyekiti wa Manchali A Bw.Manyangalazi Manyangalazi amekiri kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wake mara kwa mara kuwa kila wanapofika zahanati kupata matibabu hukumbana na ukosefu wa dawa.

Aidha Manyangalazi ameiomba serikali kupitia wizara ya Afya kuwasaidia dawa za kutosha katika zahanati hiyo ili wananchi waepukane na adha kwenda kununua dawa nje ya hospitali.

Sauti ya Bw.Manyangalazi Manyangalazi.