Dodoma FM
Dodoma FM
8 April 2026, 11:35

Changamoto ya miundombinu mibovu ya barabara imepelekea wagonjwa kushindwa kufika hospitali kwa wakati pamoja usafiri kuwa washida.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa Kijiji Cha Ndogowe wilayani Chamwino wameiomba Serikali kukarabati miundombinu ya barabara zilizo haribiwa na mvua na kupelekea adha ya usafiri.
Wakiongea na Taswira ya habari wananchi hao wamesema mvua za masika zilizo nyesha mfululizo zimepeleakea barabara ya eneo hilo kuwa na mashimo pamoja na kutengeneza madimbwi ya maji hali inayokwamisha usafiri katika eneo hilo.
Aidha wamesema changamoto ya miundombinu mibovu ya barabara imepelekea wagonjwa kushindwa kufika hospitali kwa wakati pamoja usafiri kuwa washida.
Keneth Muhawi mwenyekiti wa Kijiji hicho amekiri uwepo wa adha ya miundombinu ya barabara iliyochangiwa na mvua zilizo kuwa kikiendelea kunyesha