Dodoma FM

Mchakato wa mabinti walio jifungua kurudi shule jamii bado ipo gizani

2 April 2026, 17:25

Unyanyapaa pia ni sababu kubwa inayo wafanya mabinti wengi walio jifungua kushindwa kurudi kuendelea na masomo.Picha na Mtandao.

Mwaka 2022 serikali ilitoa waraka wa wananafunzi wa kike wanaopata ujauzito kurejea mala baada ya kujifungua .

Na Steven Noel.

Wadau wa Elimu Katika kata nne za wilaya ya Mpwapwa wamesema Bado mkakati uliotolewa na serikali  wa kuwarejesha shule Wanafunzi waliopata ujauzito Bado haueleweki Kwa Jamii.

Wakijadili kwenye kikao cha Siku mbili kilichodhaminiwa na shirika la Haki Elimu wadau wa Elimu kutoka kata za Mazae,Mpwapwa mjini ,Godegode na Pwaga  wamesema pamoja na serikali kutoa waraka huo wa mwaka 2022 lakini Bado uelewa wa jamii ni mdogo juu kuwarejesha shuleni mabinti hao.

Aidha wamesema sababu zingine ni pamoja na  mlolongo mrefu wa ufuatiliaji wa urejeaji shule ambao unasababisha baadhi ya wazazi kukata tamaa.

Kwa upande wake Afisa kutoka shirika la Haki Elimu Dkt ,Wilbafoce Meena  amesema tafiti zilizofanywa na shirika lake zimebaini uelewa mdogo wa jamii,unyanyapaa ulipo  Kwa baadhi walimu na Wanafunzi Kwa mabinti waliopata ujauzito nazo ni sababu zinazopelekea wengi kushidwa kurudi.

Sauti ya kina Noel.