Dodoma FM

Wananchi watakiwa kujihadhari dhidi ya kifua kikuu

24 March 2026, 16:31

ugonjwa wa kifua kikuu huenezwa kwa njia ya hewa na unatibika na dawa zinatolewa bure.Picha na michuzi blog.

Ikumbukwe kuwa kila ifikapo March 24 kila mwaka Dunia huazimisha siku ya kifua kikuu.

Na Jerome john.

Wananchi  Mkoani  Dodoma wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu wawapo kwenye mazingira ya kufanyia kazi au nyumbani.

Akizungumza na Taswira ya Habari mratibu wa kifua kikuu na ukoma mkoani Dodoma Dkt Peres Lukango amesema kuwa ugonjwa wa kifua kikuu huenezwa kwa njia ya hewa na unatibika na dawa zinatolewa bure kuanzia ngazi za zahanati hadi hospital kuu zote nchini.

Aidha Dkt Peres amebainisha kuwa kulingana na takwimu za kitaifa za mwaka jana juu ya ugonjwa wa kifua kikuu mkoa wa Dodoma ulibainika kuwa na wagonjwa 7800,huku maambukizi kwa watoto yakionekana kuwepo miongoni mwao.

Vile vile mtaalamu huyo ameitaka jamii kuzingatia lishe bora kwa ujumla ili kuupa mwili kinga kamili kupitia lishe na kuweza kuwa na uwezo wa kutopata maambukizi kwa urahisi na kuzuia unyemelezi wa magonjwa ikiwemo kifua kikuu.

Sauti ya Dkt Peres .

Ikumbukwe kuwa kila ifikapo March 24 kila mwaka Dunia huazimisha siku ya kifua kikuu kutokana na mikakati mbalimbali inayowekwa ili kudhibiti ugonjwa huo, kaulimbiu ya mwaka huu ni kwajitihada za viongozi,wadau na wananchi tunaweza kutokomeza kifua kikuu nchini.