Dodoma FM
Dodoma FM
23 March 2026, 18:48

Na Mariam Kasawa.
Kuzuia uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji kunahitaji ushirikiano wa jamii, serikali, na taasisi kupanda miti, kulinda misitu, na kudhibiti taka. Hatua muhimu ni pamoja na sheria kali za mazingira (Sura 191), kutoa elimu, na kusimamia mipango kabambe ya hifadhi ili kuzuia ukame na uchafuzi wa mito na maziwa.
Licha ya kuwepo na Sheria za Usimamizi wa vyanzo vya maji (bahari, maziwa, mito, mabwawa, na chemichemi) kumekuwepo na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji kutokana na kuwepo kwa shughuli za binadamu zinazofanyika pasipo kiuzingatia Sheria zinazosimamia mazingira na rasilimali maji.
Shughuli hizo ni pamoja na ukataji wa miti kwa ajili ya kujipatia kuni, mkaa au mahitaji ya ujenzi, mifugo, uchimbaji mchanga na madini, na ujenzi usiozingatia taratibu taratibu za mipango miji, kilimo kisicho endelevu.
Pia shughuli za uchimbaji mchanga kwenye maeneo ya mito na uchimbaji madini kwenye vyanzo vya maji, kilimo na maogesho ya mifugo katika vyanzo hivyo vimekuwa vikichangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa vyanzo vya maji hususani kuongeza matope kwenye vyanzo vya maji.
Vilevile uchepushaji wa maji kutoka katika vyanzo vya maji pasipo kuzingatia sheria na taratabu zilizowekwa na serikali za uchukuaji maji kwenye vyanzo vya maji (wenye vibali vya kuchota maji kuchukua maji zaidi ya viwango vilivyoidhinishwa).