Dodoma FM

Wananchi Muungano watakiwa kulipa bili za maji

23 March 2026, 18:22

Ni wajibu wa Kila mwananchi aliyevuta huduma ya maji nyumbani kwake kulipia bili.Picha na Mtandao.

Licha ya changamoto ya baadhi ya miundombinu ya maji kijijini hapo lakini kumeibuka tabia ya baadhi ya wananchi kushindwa kulipa bili za maji za kila mwezi hali inayo kwamisha uendeshaji wa huduma hiyo.

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa Kijiji Cha Muungano na Vitongoji vyake wametakiwa kulipia bili za maji Ili kusaidia uendeshaji wa huduma hiyo muhimu Kwa jamii

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Matonya Mtukamsihi ambaye amesema kuwa licha ya changamoto ya baadhi ya miundombinu ya maji kijijini hapo lakini kumeibuka tabia ya baadhi ya

Mtukamsihi ameongeza kuwa ni wajibu wa Kila mwananchi aliyevuta huduma ya maji nyumbani kwake kulipia bili .

Sauti ya Bw.Matonya Mtukamsihi

Aidha amewataka wasimamizi wa mradi kuhakikisha wanashirikiana na viongozi wa Serikali ya mtaa katika kusimamia na kuendesha mradi huo Ili kukabiliana na changamoto kama hizo.

Sauti ya Bw.Matonya Mtukamsihi

Nao baadhi ya wakazi wa Muungano wamesema kuwa changamoto ya kugoma kulipa bili za maji inatokana na ubovu wa mita walizo fungiwa kwani gharama wanazo paswa  kulipa huwa ni kubwa tofauti na matumizi ya maji wanayo tumia kila siku.

Sauti za wananchi.