Dodoma FM
Dodoma FM
23 March 2026, 17:27

Ameeleza kuwa suala hilo tayari liliwasilishwa kwa Mkurugenzi wa Jiji ambapo uchimbaji ulisitishwa kwa muda, lakini baadaye ukaendelea tena.
Na Mariam Kasawa.
Diwani wa Kata ya Zuzu, Jenesta Project Malingo, amesema anaendelea kufuatilia malalamiko ya wananchi wa Mtaa wa Sokoine waliotaka kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji wa madini ya ujenzi.
Akizungumza katika mahojiano na moja ya chombo cha habari hapa jijini Dodoma amesema wananchi wanalalamikia uchimbaji huo kusababisha mashimo makubwa yanayohatarisha usalama wao.