Dodoma FM
Dodoma FM
20 March 2026, 16:23

Alisema wanatarajia kuendelea kuinua kiwango cha taaluma na kuhakikisha wanafunzi wanapanda daraja mwaka hadi mwaka.
Na Mariam Kasawa.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makutupora watakiwa kuwa na nidhamu na kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao ya kielimu na maisha kwa ujumla.
Hayo aliyasema Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani la Tanzania, Prof. Said Mohamed wakati wa Uzinduzi wa Upandaji Miti mwaka 2025/2026 uliofanyika katika Shule ya Sekondari Makutupora Jijini Dodoma.
Alisema kuwa juhudi za wanafunzi katika masomo ni msingi muhimu wa maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla.
Aidha aliwapongeza wazazi kwa juhudi wanazozifanya katika malezi ya watoto.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Makutupora, Mwl. Didas Ndalu alimshukuru Katibu Mtendaji kwa kutembelea shule hiyo akieleza kuwa ujio wake ni faraja kubwa kwa wanafunzi na walimu.
Kutokana na walimu kuendelea kusimamia nidhamu ya wanafunzi ufaulu umeendelea kuongezeka ikiwa kwa mwaka 2025 shule ilifaulu kwa GPA ya 3.4842, lakini pia tunaendela kuweka mikakati ya kuhakikisha tunafuta daraja sifuri na nne.
Nae mzazi alieshiriki katika uzinduzi wa upandaji miti, Phatina Mbeyu alisema kuwa wazazi wataendelea kushirikiana na walimu katika kuhakikisha watoto wanalelewa katika maadili mema.