Dodoma FM

Washikiri zoezi la upandaji miti Shule ya Mzingi Mchemwa

19/03/2026, 16:35

Shule ya Msingi Mchemwa ilipokea jumla ya miche 1,000 ya miti kutoka Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwaajili ya kuipanda.Picha na Dodoma cc news.

Umuhimu wa kupanda miti na kutunza mazingira ya shule una faida nyingi kama vile kupata miti ya kivuli, kuchangia katika kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na kukuza elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa wanafunzi na jamii.

Na Mariam Kasawa.

Uongozi wa Kanda namba Sita katika Manisipaa ya Dodoma wameshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Shule ya Mzingi Mchemwa ukiwa na lengo la kuhimiza utunzaji wa mazingira na kuondokana na athari za mvua na joto kali.

Shule ya Msingi Mchemwa ilipokea jumla ya miche 1,000 ya miti kutoka Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwaajili ya kuipanda ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani ambapo Shirika la Habitat for Humanity Tanzania kwa kushirikiana na wataalam wa mazingira kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma walishiriki katika zoezi la kupokea na kupanda miti katika shule ya hiyo.

Aina na idadi ya miti iliyopandwa ni Bauhinia muricata (Mti Kipepeo) 100, Acacia nilotica (Migunga) 300, Syzygium cumini (Mzambarau) 200, Trichilia emetica (Miti Maji) 300, Jacaranda mimosifolia (Mjakaranda) 50 na Melia azedarach (Mwarobaini dume) 50.