Dodoma FM

Tume ya utumishi kutumia wiki mbili kuamua rufaa za watumishi

19/03/2026, 16:02

Tume itapitia taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya tume. Picha na Mtandao.

Tume ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itawalisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya tume, kujadili na kutolea maelekezo kwenye mkutano wake.

Na Anwary Shaban.

Tume ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imepanga kujadili  malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa na watumishi wa umma kuanzia Machi  23 Aprili 15 .

Hayo yamesemwa na kaimu katibu wa Tume hiyo  John Mbisso  jijini Dodoma  wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa mkutano huo utalenga kujadili rufaa na malalamiko ya watumishi wa umma .

Sauti ya John Mbisso.

Aidha katika mkutano huo Tume itapitia taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya tume pamoja na kuwasilisha taarifa na kuzijadili.

Sauti ya John Mbisso.