Dodoma FM

Mwekezaji  Muungano ashindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi

17/03/2026, 18:20

licha ya uzalishaji wa kokoto kuendelea katika kijiji hicho lakini ahadi hazijatekelezeka hadi leo.Picha na Mtandao.

Juhudi za kumpata Ndg.Baraka Baradiga GG maining Company ambaye ndiyo mmiliki wa kampuni ya kusaga kokoto katika mgodi huo hazikufanikiwa.

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa Kijiji Cha Muungano Wilaya ya Chamwino wamesikitishwa na mwekezaji wa madini na kokoto wa eneo hilo  kushindwa kufuata mkataba walio wekeana kati ya kijiji na mwekezaji huyo.

Wakiongea na taswira ya habari wananchi hao wamesema mwekezaji huyo aliingia makubaliano na kijiji hicho ya kujenga vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari pamoja na jingo la ofisi ya kijiji lakini hajawahi kutekeleza ahadi hiyo .

Aidha wananchi hao wamesema kuwa wamekuwa wakiitisha vikao na mwekezaji huyo mara kwa mara ili kumkumbusha kutekeleza ahadi hiyo lakini amekuwa hatekelezi lolote hivyo wanaiomba serikali kuingilia kati suala hilo.

Sauti za wananchi.

Matonya Mtukamsihi mwenyekiti wa Kijiji Cha Muungano amekiri uwepo wa changamoto hiyo katika uwekezaji wa madini kokoto Kutokana na mwekezaji huyo kushindwa kufuata mkataba walio kubaliana nae.

Sauti ya Matonya Mtukamsihi

Mtukamsihi amesema licha ya uzalishaji wa kokoto kuendelea katika kijiji hicho lakini mwekezaji huyo ameshindwa kutimiza ahadi aliyo wapa wakazi wa eneo hilo ya kujenga vyumba vya madarasa na ofisi ya kijiji.

Sauti ya Matonya Mtukamsihi