Dodoma FM
Dodoma FM
17 March 2026, 17:22

Kuharibika kwa miundombinu ya Barabara katika kipindi hiki cha masika ni suala ambalo limekuwa likiripotiwa katika maeneo mbalimbali nchini ambapo serikali inaendelea na juhudi za kuboresha miundombinu ili kukabiliana na hali hiyo.
Na Amina Juma.
Ubovu wa miundombinu ya Barabara katika mtaa wa miyuji kata miyuji jijini Dodoma umeendelea kuathiri kipato kwa maafisa usafirishaji maarufu kama boda boda hususani katika kipindi hiki cha mvua ambazo zinanyesha maeneo mbalimbali nchini.
Wakizungumza na Dodoma Fm baadhi ya wakazi katika mtaa huo wamesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha athari kubwa ikiwepo uharibifu wa miundombinu ya Barabara katika kata ya miyuji.
Kuharibika kwa miundombinu hiyo kumepelekea baadhi ya maafisa usafirishaji kushindwa kufanya shughuli za usafirishaji hali inayo wakosesha kipato chao cha kila siku.
Nao baadhi ya wakazi wa mtaa wa Miyuji wameiomba serikali kuhakikisha inafanya maboresho ya miundombinu ya Barabara ili kuepuka maji kutuama katika barabara kipindi hiki cha mvua kwani ni hatari kwao.