Dodoma FM
Dodoma FM
17/03/2026, 16:39

Kituo hicho kinatarajiwa kurahisisha utoaji wa huduma za kisheria kwa wananchi kote nchini, huku kikiwapa fursa ya kuwasilisha malalamiko na kupata msaada wa haraka kupitia namba za simu za bure 026 216 0360 au 0800 004 004.
Na Bennard Komba.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Homera, amezindua rasmi kituo cha huduma kwa mteja chenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto za kisheria zinazo wakabili wananchi nchini.
Uzinduzi huo umefanyika leo Machi 17, 2026, katika makao makuu ya Wizara ya Katiba na Sheria, yaliyopo Mtumba jijini Dodoma.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Dkt. Homera amesema kumekuwepo na ongezeko la wananchi wanao kumbana na changamoto mbalimbali za kisheria, hali inayo lifanya kuwa muhimu kuanzishwa kwa kituo hicho ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na kuwaelekeza wananchi kwenye mamlaka husika kwa utatuzi.

Aidha, Dkt. Homera amesematangukuanzishwakwakituohichoFebruari 14, 2024, tayarikimepokeanakushughulikiajumlayachangamoto 2,023, nyingizikiwazinahusumasualayandoa, ardhi, talaka, kazinaajirapamojanamatunzoyawatoto.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Zainabu Katimba, amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan, yanayolenga kuboresha utoaji wa huduma za serikali kwa kutumia mifumo ya kidijitali ili kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi.