Dodoma FM

Walio vamia eneo la kimila Mapinduzi A watakiwa kuondoka mara moja

02/03/2026, 17:45

Eneo hilo lilitengwa Ili kusaidia kuendesha tamaduni za jamii yao ya wagogo ,kulinda miti mkubwa ya asili pamoja na kutunza maadili Kwa vijana.Picha na mtandao.

Wananchi wote walio vamia na kujikatia vipande katika eneo hilo kabla ya kusubiri kutolewa na mamlaka wametakiwa kuondoka mara moja.

Na Victor Chigwada.

Imeelezwa kuwa hapo awali ili kulinda mazingira ya eneo la kimila Kwa wakazi wa Mapinduzi A waliunda baraza la kusimamia eneo hilo Kwa tahadhari ili lisiathiriwe na shughuli za kibinadamu .

Taswira ya habari baada ya kufanya mazungumzo na wakazi wa eneo la Mapinduzi A sanjali na Mwenyekiti wao wa mtaa ilibaini uwepo wa baadhi ya wananchi kupuuza eneo hilo na kulivamia Kwa shughuli zao binafsi.

Hali hii ilitulazimu kumtafuta Moja ya viongozi wa kamati ya mazingira ya eneo la kimila ambaye ndiye alikuwa katibu wa baraza Hilo Bw.Lazaro Maguho ambapo amesema eneo hilo lilitengwa Ili kusaidia kuendesha tamaduni za jamii yao ya wagogo ,kulinda miti mkubwa ya asili pamoja na kutunza maadili Kwa vijana wanapo fikia umri wa kwenda jando.

Sauti ya Bw.Lazaro Maguho.

Ameongeza kuwa eneo hilo liliaminiwa na kijiji kizima Cha Mapinduzi A na maeneo ya vijiji jirani kwani ilipo fika kipindi Cha jando zaidi ya vijana wa vijiji vinne vilikutana katika eneo hilo la kimila kufanya tohara na matambiko.

Sauti ya Bw.Lazaro Maguho.