Dodoma FM

Wawezeshaji sekondari watakiwa kuwa na nidhamu na uwajibikaji shuleni

02/03/2026, 16:52

Mwezeshaji wa Stadi za Maisha wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Tuvacal Mjema.Picha na Jiji la Dodoma.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwajengea wanafunzi maarifa, ujuzi na mitazamo chanya itakayowawezesha kujitambua, kujiamini na kufanya maamuzi sahihi.

Na Mariam Kasawa.

Wawezeshaji wa Stadi za Maisha katika Shule za Sekondari watakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika taaluma yao ikiwemo kuwajibika ipasavyo pamoja na kutumia mafunzo waliyoyapata kuleta mabadiliko chanya kwa wanafunzi.

Hayo yalisemwa na Mwezeshaji wa Stadi za Maisha wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Tuvacal Mjema baada ya kupokea mafunzo ya Elimu ya Stadi za Maisha yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma jijini Dodoma.

Picha ni mafunzo ya Elimu ya Stadi za Maisha yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma jijini Dodoma.Picha na Jiji la Dodoma.

Alisema kuwa wawezeshaji wanapaswa kuwa mfano bora kwa wanafunzi kwa kuzingatia maadili, kuwajibika ipasavyo na kuonyesha weledi katika utekelezaji wa majukumu yao. “Ni muhimu kwa wawezeshaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu wanapokuwa shuleni.

Alimalizia kwa kusema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwaongezea uwezo wa kitaaluma na kisaikolojia wawezeshaji ili waweze kuwasaidia wanafunzi. “Kupitia mafunzo haya ninaamini kuwa tunawaongezea walimu ujuzi ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za wanafunzi zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku na masomo kwa ujumla” alimalizia Mjema.

Kwa upande wake, Mwezeshaji wa Stadi za Maisha katika Shule ya Sekondari Miyuji, Sophia Kasekwa alisema kuwa kupitia mafunzo hayo wamepata maarifa na mbinu zitakazowawezesha kuwafikia wanafunzi kwa ufanisi zaidi.