Dodoma FM

Chinyika waiomba serikali kutatua kero ya maji

27 February 2026, 17:03

Serikali ipo kwenye mikakati ya kutatua changamoto hii ya maji.Picha na Wizara ya maji.

Aidha amewahimiza wakazi wa Chinyika wajitokeze kwa wingi katika mkutano utakaofanyika kesho

Na Farashuu Abdallah.

Wakazi wa mtaa wa Chinyika kata ya Mkonze jijini Dodoma wameiomba serikali kutatua changamoto ya maji ambayo imekuwa ni kero ya muda mrefu.

Wakizungumza na Dodoma Fm baadhi ya  wananchi hao wamesema changamoto hiyo ya maji imekuwepo tangu mwaka 2023 ambapo wamekuwa wakitegemea kisima kimoja huku wakiiomba Serikali iwatatulie changamoto hiyo.

Sauti mwananchi

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Chinyika Bw.Kombo Ally Kombo ametolea ufafanuzi changamoto hiyo ambapo amesema  Serikali ipo kwenye mikakati ya kutatua changamoto hii.

Sauti ya Bw.Bw.Kombo Ally

Aidha amewahimiza wakazi wa Chinyika wajitokeze kwa wingi katika mkutano utakaofanyika kesho wenye lengo la kuzungumzia mustakabali wa changamoto hiyo.

Sauti ya Bw.Bw.Kombo Ally