Dodoma FM

Wakazi walia na uharibifu wa mazingira

19/02/2026, 16:24

Picha ni eneo uharibifu ulio fanywa na mvua katika eneo hilo.Picha na Steven Noel.

Viongozi wa eneo hilo wamelalamikiwa kushindwa kuwachukulia hatua wahusika wa uharibifu wa mazingira hayo.

Na Steven Noel.

WAKAZI WA Kitongoji cha Mcheula Kijiji cha Idilo kata ya Mazae wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wamelalamikia matokeo ya uharibifu wa mazingira  katika milima ya Idilo na Nguji kutokana na baadhi ya watu kuendesha kilimo katika milima hiyo bila kuchukuliwa hatua .

Wakiongea na Taswira ya Dodoma Fm  baadhi ya wakazi wa Kitongoji hicho wamewalalamikia viongozi waliopewa mamlaka kushindwa kuwachukulia hatua wahusika wa uharibifu wa mazingira hayo .

Ezely Chalio, mwenyekiti  wa Kitongoji  cha Mcheula  amekiri  kuwepo Kwa baadhi ya wananchi ambao mashamba yao yamsombwa na maji na hivyo kuwasababishia  hasara kubwa.

Sauti ya kina.