Dodoma FM
Dodoma FM
10 February 2026, 11:51 am

Hayo yana jiri ikiwa ni siku chache tangu familia moja kuibiwa Ngombe wote walio kuwa zizini katika kitongoji Cha Ilolo kata ya Ihumwa.
Na Victor Chigwada.
Changamoto ya wizi wa mifugo imebua sauti za wakazi wa Mtaa wa Ihumwa na viunga vya jirani zikiwa na lengo la kupata Suluhu ya kukomesha wizi wa mifugo.
Wakieleza kadhia hiyo wananchi hao wamesema ni zaidi ya miaka mitatu changamoto ya wizi wa mifugo imekuwa ikiwakabili katika eneo hilo bila kupatiwa suluhisho lolote licha ya viongozi wa eneo hilo kufahamu changamoto hiyo.
Aidha wameongeza kuwa ni vema Serikali ikachukua hatua mapema za kudhibiti wizi huo wa mifugo kwa kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa mifugo yote inayo ingia na kutoka ndani ya mtaa.
Taswira ya habari imemtafuta mwenyekiti wa mtaa wa Ihumwa Bw.Lameck Mbinda ambapo amesema kuwa changamoto ya wizi wa mifugo katika eneo hilo imekuwa ni ngumu kukabiliana nayo kutokana na baadhi ya watu kushindwa kuchukua hatua stahiki pindi wanapo wadhibiti wezi hao kwani baadhi ya wezi wanatoka katika familia zao.