Dodoma FM

Madiwani Mpwapwa waijia juu TARURA

4 February 2026, 12:14 pm

Picha ni Meneja wa TARURA wilaya ya Mpwapwa Muhandisi Emanuel Lukumay akiongea na taswira ya habari baada ya kikao hicho.Picha na Steven Noel.

TARURA imetakiwa kuzingatia upangaji wa majeti ili kurahisisha wilaya hiyo kuboreshewa miundombinu kwa urahisi.

Na Steven Noel.
Baraza la madiwani Katika halmashauri ya Mpwapwa waitaka Wakala wa barabara vijijini TURURA wilayani humo kuzingatia upangaji wa bajeti zao kutokana na uhitaji wa maeneo magumu Ili kuweza kuifungua wilaya kimawasiliano.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo kwenye kikao cha kupitisha bajeti ya halmashauri kilicho fanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Meneja wa TARURA wilaya ya Mpwapwa Muhandisi Emanuel Lukumay amekiri kuwepo Kwa changamoto za barabara ambazo hazipitiki hasa msimu wa mvua ambapo amesema umesababishwa na barabara nyingi kuharibiwa na maji na baadhi ya vivuko kukatika .

Aidha amesema mkakati wa Ofisi za kuzikarabati njia zote za TARURA ambazo zimeharibiwa na mvua Ili kumrejesha mawasiliano.

Naye mwenyeki wa halmashauri hiyo bwana Richard Maponda ameitumia fursa hiyo kuishauri TARURA kuyazingatia maeneo yaliyo haribiwa miundombinu kwa kiasi kikubwa.