Dodoma FM
Dodoma FM
7 August 2025, 1:41 pm

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Zanzibar, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sitti Ali ameishuruku Wizara ya Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum kwa kufanikisha ushiriki.
Na Mariam Matundu.
Waratibu wa Programu ya Kizazi chenye Usawa wametakiwa kuhakikisha wanakusanya taarifa zenye matukio chanya na changamoto zake na kuzichakata vizuri kwa ajili ya kurahisisha uaandaaji wa taarifa ya ujumla ya kitaifa.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Programu ya Kizazi chenye Usawa Mhe. Angela Kairuki jijini Dodoma wakati wa kuhitimisha Kongamano la Tathimini ya Utekelezaji wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa ngazi ya Mikoa na Hamashauri lililohudhuriwa na Maafisa Maendeleo ya Jamii ambao ni waratibu wa Programu hiyo kutoka katika Halamashauri na Mikoa yote ya Tanzania pamoja na Wawakilishi kutoka Zanzibar.

Kairuki ameeleza kuwa Programu hiyo inatarajia kufikia ukomo ifikapo Juni 2026 kwani huo ndiyo wakati muafaka ambapo jamii itatakiwa kufiki namna bora ya kuiendeleza ili kuimarisha usawa wa kijinsia na haki za kiuchumi kwa wanawake na wasichana kwenye kwenye halmashauri na mikoa pamoja na kushirikiana na vyombo vya habari kwa ajili ya kuwa na hadithi nzuri kuhusu Programu hiyo.
Aidha, Kairuki ametoa msisitizo kwa waratibu katika baadhi ya maeneo ambapo amegusia juu ya uzingatiaji wa malengo ya Programu ili kuhakikisha kunakua na uendelevu, kuhakikisha waratibu wanafanya thathimini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa Programu pamoja kukamilisha taarifa zao, kudumisha ushirikiano na wadau hasa wa Asasi za kiraia, kijamii na makundi mengine ili kuweza kukamilisha malengo yaliyowekwa na kuanzisha utaratibu na utamaduni wa kujifunza baina ya Waratibu.