Dodoma FM

Leo tunaangazia kwa namna gani tunaweza kuondoa changamoto kwa msichana aliyejifungua kurudi shule.

29 January 2025, 4:01 pm

mwaka 2022, wanafunzi wa kike 66,466 wa sekondari na 81,239 wa shule za msingi waliacha shule nchini Tanzania.Picha na Global Tv.

Na Seleman Kodima.
Elimu ni msingi muhimu kwa maendeleo ya jamii na uchumi wa nchi yoyote. Hata hivyo, takwimu za Ofisi ya Rais Tamisemi zinaonyesha kwamba mwaka 2022, wanafunzi wa kike 66,466 wa sekondari na 81,239 wa shule za msingi waliacha shule nchini Tanzania.

Hii ni idadi kubwa inayosababisha wasiwasi kuhusu mustakabali wa elimu kwa wasichana nchini. Licha ya jitihada za serikali, changamoto nyingi bado zinakwamisha wanafunzi wa kike kuendelea na masomo baada ya kukatizwa na sababu mbalimbali, ikiwemo ujauzito.

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alianzisha sera inayoruhusu wanafunzi wa kike waliopata ujauzito wakiwa shuleni kurejea kuendelea na masomo. Sera hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha haki ya elimu kwa wasichana, lakini utekelezaji wake unakutana na vikwazo mbalimbali.

Ripoti ya Shirika la Haki Elimu ya mwaka 2024 imetaja sababu zinazoathiri uwezo wa wasichana waliojifungua kurudi shule, ikionyesha jinsi vikwazo vya kijamii, kiuchumi na kisaikolojia vinavyoweza kuwa vizuizi vikubwa.

Leo Mwandishi wetu Selemani Kodima ametuandalia taarifa ifuatayo kuhusu mwalimu aliyeweza kumsaidia msichana aliyekatiza masomo kutokana na kupata mimba ambaye baadae alijifungua na kurudi shuleni.