RC Kagera azindua mafunzo kwa wanahabari juu ya ugonjwa wa marburg
29 January 2025, 1:38 pm
Upo umhimu mkubwa kwa redio jamii kushikiri kuhamasisha jamii juu ya namna na kukabiliana na ugonjwa.
Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Hajjat Fatma Abubakari Mwassa, amezindua rasmi semina ya mafunzo ya siku nne kwa waandishi wa habari wapatao 100, yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika na kuripoti kwa usahihi habari zinazohusiana na magonjwa ya mlipuko, hususan ugonjwa wa Marburg.
Katika hotuba yake akifungua mafunzo hayo, Mhe. Mwassa alisisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuwa na taarifa sahihi na za kina ili kuhakikisha umma unapata uelewa mzuri kuhusu hatua za kinga, kudhibiti hofu, na kuimarisha uhamasishaji wa afya ya jamii.
Mafunzo haya yana lengo la kuhakikisha vyombo vya habari vinakuwa wabia wa karibu wa sekta ya afya kwa kuwasilisha taarifa kwa usahihi na kwa namna inayosaidia kudhibiti hofu, kuongeza uelewa wa jamii, na kuchochea hatua za kinga dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
Wataalamu wa afya na washirika mbalimbali pia wanashiriki kuongoza mafunzo haya, yakitarajiwa kuleta matokeo chanya katika kupambana na changamoto za afya ya umma.
Mafunzo hayo ya siku nne yameanza tarehe 28 Januari 2025 katika hoteli ya ELCT, Manispaa ya Bukoba yakiwakutanisha Jumla ya waandishi wa habari 100 kutoka radio jamii wanachana wa TADIO na vyombo vyengine wamepatiwa mafunzo hayo huku shughuli nzima ikiongozwa na Mwenyekiti wa RADIO Jami Tanzania TADIO ambae pia ni mkurugenzi ya Dodoma Media Group inayo miliki vituo vya Dodoma FM Dodoma Tv na Km24 Fm ya Kahama Bw Baptis John Mutesasira.
Mafunzo hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulika na watoto duniani- UNICEF, Wizara ya Afya, Mtandao wa vyombo vya habari vya kijamii Tanzania- TADIO , na wadau wengine wa maendeleo.
Aidha Mwenyekiti wa RADIO Jami Tanzania TADIO ambae pia ni mkurugenzi ya Dodoma Media Group inayo miliki vituo vya Dodoma FM Dodoma Tv na Km24 Fm ya Kahama amesema upo umhimu mkubwa kwa redio jamii kushikiri kuhamasisha jamii juu ya namna na kukabiliana na ugonjwa huo kwa kutoa elimu kupitia kwa wataama wa afya.