Dodoma FM
Bahi kuongeza pato ujenzi vibanda vya biashara
14 October 2024, 7:56 pm
Na Leonard Mwacha.
Wilaya ya Bahi inatarajiwa kuongeza pato lake la ndani kutokana na ushuru wa vibanda vya biashara pamoja na ushuru wa bishara ndogo ndogo.
Bwn. Jeremia Maximilian mjumbe ngazi ya ustawi wa jamii Bahi sokoni amesema eneo ambalo litatumika kwa ajili ya ujenzi wa vibanda na biashara ndogo ndogo hapo litasaidia kuleta maendeleo katika ngazi ya kijiji.
Aidha wafanyabiashara ndogo ndogo wamepongeza hatua ya iliyofikiwa na kufanya eneo hilo kuwa ni sehemu ya biashara na kwani itawaondolea adha ya kufanya biashara tembezi.