Dodoma FM

Wananchi Dodoma washauri suluhisho migogoro ya ardhi

2 October 2024, 8:57 pm

Na Nazael Mkude.

Wakazi wa mkoa wa Dodoma wametoa  maoni yao kuhusu njia za kupunguza migogoro ya ardhi katika jiji la Dodoma.

Wakizungumza na Dodoma TV, Wakazi hao wamesema kuwa  ili kupunguza migogoro ya ardhi inapaswa  viongozi na wananchi kushirikiana kwa kupitaa njia shirikishi ya mikutano ya hadhara .

Pichani mkazi wa jijini la Dodoma akieleza ushauri wake kuhusu suluhisho la migogoro ya ardhi
Sauti za wananchi
Pichani mkazi wa jijini la Dodoma akieleza ushauri wake kuhusu suluhisho la migogoro ya ardhi

Katibu wa wenyeviti na vitongoji nchini Bwn. John Komba amesema ili kumaliza migogoro ni jukumu la wananchi kuwa makini hasa katika kununua eneo na kutambua ramani ya jiji ili kuepuka usumbusu.

Katibu wa wenyeviti wa vitongoji nchini Bwn. John Komba
Sauti ya Bwn. John Komba