Wanaume tumieni dawati la jinsia kuripoti ukatili
25 September 2024, 8:26 pm
Na Lilian Leopold
Licha ya kampeni za kupinga ukatili kufanyika hususani kwa wanawake, watoto na watu wenye ulemavu lakini wanaume wamekuwa wakisahaulika.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi mkoa wa Dodoma, Michael Nkinda amesema kuwa wanaume wengi wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa kijinsia unaopelekea kupata ukatili wa kisaikolojia.
Aidha ametoa wito kwa wanaume wanaofanyiwa ukatili kwenye jamii wasione aibu kupaza sauti zao hasa kwenye mamlaka husika hususani katika Dawati la Jinsia ili changamoto zao ziweze kutatuliwa na kuleta usawa katika jamii.
Baadhi ya wanaume jijini Dodoma wametoa maoni yao juu ya nini cha kufanya endapo wanaume wanakabiliwa na ukatikli wa kijinsia.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2023, vitendo vya ukatili kwa wanaume vimeongezeka na kufikia asilimia 10, kutoka asilimia 6 ya mwaka 2022.