Dodoma FM

Nguvu ya maombi yamtungua bundi wa ajabu kanisani

13 September 2024, 7:30 pm

Picha ya bundi wa ajabu akiwa ameanguka katika eneo la kanisa

Wakazi wa mtaa wa Maili Mbili CCM wameonesha mshangao baada ya kuona bundi huyo ameanguka kwenye eneo la kanisa akiwa na vifaa mabilimbali vya kiuchawi.

Na Thadei Tesha.

Wakazi wa Mtaa wa Maili Mbili  CCM jijini Dodoma wameshudia tukio la ajabu linalohusisha  kuanguka kwa ndege jamii ya bundi kwenye maeneo ya kanisa

Bi Frida Maiko akisimulia tukio la bundi kuanguka
Sauti ya Bi Frida Maiko

Akisimulia mkasa huo mkazi mmoja aliyejulikana kwa jina la Bibi wa Taifa, alitilia shaka juu ya muonekano wa bundi kufananisha na bundi wa kawaida na pia kueleza zaidi juu ya vitu  walivyoviona katika eneo alipoanguka bundi huyo.

Sauti ya Bibi wa Taifa

Wakazi hao wameonesha mshangao baada ya kuona bundi huyo ameanguka kwenye eneo la kanisa na akiwa na vifaa mabilimbali vya kiuchawi. Inaelezwa kuwa moja ya vitu  walivyoviona ni pamoja na chupa yenye damu mbichi .

Bi Dafrosa Lewis akielezea tukio la kuanhuka kwa bundi kanisani baada ya maombi ya mkesha
Sauti ya Bi Dafrosa Lewis

Bi. Dafrosa Lewis mbaye ni moja ya muumini ambaye alishiriki maombi ya mkesha katika kanisa kale siku ya Ijumaa ambapo usiku huo mchungaji wao aliwataka kuomba ili kupambana na  vitu visivyoeleweka vinavyozunguka juu ya anga maeneo ya kanisa mwishoni mwa wiki jana.

Pichani ni ungo mweusi ikiwa ni moja ya kifaa kilichokutwa eneo la tukio
Picha kuonesha bundi akiwa na vifaa vya kichawi