Dodoma FM

Wananchi walilia fidia ya maeneo ndani ya mradi wa SGR

4 September 2024, 7:04 pm

Wananchi wanaoishi katika eneo la Image Jijini Dodoma wameonesha wasiwasi wa kutopata stahiki ya fidia

Wananchi walilia fidia ya maeneo ndani ya mradi wa SGR

Na Mindi Joseph. Wananchi wanaoishi katika eneo la Image Jijini Dodoma wameonesha wasiwasi wa kutopata stahiki ya fidia yenye tija kutokana na maeneo yao yaliyo ndani ya mradi wa SGR kutomilikishwa kwa utaratibu wa Kiserikali.

Wananchi hao wamesema wamekabiliwa na changamoto ya kutopimiwa maeneo yao kwa kipindi cha miaka 12. Hivyo wanaomba wameiomba Serikali kuwamiliksha kisheria ili waweze kulipwa fidia stahiki kulingana na thamani ya maeneo hayo.

Aidha kwa upande mwingine Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Ndg. Jawadu Mohammed  amewahakikishia wananchi hao kuwa kilio chao kimefika mahala sahihi kwani yupo tayari kushughulikia suala hilo.