Dodoma FM

Kazi ya ushonaji kofia ilivyorithishwa kwa watoto Kingale

15 August 2024, 6:22 pm

Picha ni kofia ambayo imefumwa kwa mkono. Picha na Fahari ya Dodoma.

Anatueleza shughuli hii ilivyomsaidia katika maisha yake na kuwalea watoto wake hadi wamefikia umri wa kujitegemea.

Na Yussuph Hassan.
Bado tunatazama ufundi wa kofia hapa kata ya Kingale ambapo mzee Ramadhani ametujuza mengi tokea alipoanza kazi hadi kuwarithisha vijana wake ujuzi huo.

pia tunajifunza pia kuwa hadi wanawake wanaweza kuitumia fursa hii na kujipatia kipato basi watoto wa mzee Ramadhani hawakuwa mbali na fursa hii kama kaka yao anavyo eleza.

Pia kwa kutumia ufundi wa mzee huyo watu wengine hususani kinamama wamekuwa pia wakitumia fursa hiyo kujiingizia kipato .